Elimu ya Fedha yafika Mbulu

MANYARA-Elimu ya Fedha imewafikia wajasiriamali na wananchi wa Mkoa wa Manyara, baada ya watumishi wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha,Bw. Salim Kimaro, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa elimu.
Mafunzo hayo yaliyolenga kuwapa uelewa wananchi kuhusu Elimu ya Fedha, imetolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya filamu yenye maudhui ya kuelimisha kuhusu namna bora ya utunzaji wa fedha binafsi, Mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba mkopo, namna bora ya kuandaa maisha ya uzeeni, umuhimu wa kuweka malengo na kusimamia malengo husika kwenye masuala ya fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news