SHINYANGA-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga juu ya shughuli za udhibiti wa huduma za nishati na maji kwa lengo la kuimarisha uelewa, leo Alhamisi Mei 2, 2024, mjini Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher amesema mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha Watanzania wanaelewa masuala ya udhibiti, haki na wajibu wao ikiwa ni katika kutekeleza kipengele cha 6(e) cha sheria ya EWURA, sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania.
Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Patrick Mabula, ameishukuru EWURA kwa semina hiyo na kuahidi elimu watakayoipata wataitumia kuelimisha wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.