Gavana Tutuba aongoza Jukwaa la Uthabiti wa Sekta ya Fedha nchini

DODOMA-Jukwaa la Uthabiti wa Sekta ya Fedha Tanzania likiongozwa na Gavana Emmanuel Tutuba, limekutana leo katika makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dodoma.
Jukwaa hilo limejadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya fedha nchini ambayo imeendelea kuwa thabiti kutokana na uwepo wa ukwasi wakutosha, kuimarika kwa shughuli za kiuchumi na kuboreshwa kwa hali ya biashara inayochochewa na sera madhubuti na hatua za udhibiti.

Aidha,jukwaa hilo linajumuisha mamlaka za uthibiti na wasimamizi wa sekta ya kifedha ikiwemo Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu.
Nyingine ni Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) na Bodi ya Bima ya Amana (DIB).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news