Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 14,2024

ARUSHA-Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda ameanza utekelezaji wa ahadi yake ya kumjengea bibi Penina Petro (70) nyumba ya vyumba vitatu na sebule huko Siwandete Kata ya Kiranyi wilayani Arusha.

Mheshimiwa Makonda aliahidi kumjenga nyumba bibi huyo wakati wa kliniki yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Arusha ambapo bibi huyo alilia mbele yake na kueleza shida ya nyumba yake kudondoka na ndugu zake kugoma kumjengea nyumba mpya.

Ni kutokana na kutojaliwa kupata mtoto na hivyo kudai kuwa hakuna haja ya kumjengea nyumba mpya,kwani hana muda mrefu wa kuendelea kuishi duniani na hatokuwa na mrithi.

Aidha,tayari wataalamu wa ujenzi wamefika kwenye eneo la bibi huyo kwa ajili ya upembuzi wa awali na kupima eneo hilo na kulingana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ujenzi wa nyumba hiyo unatarajiwa kuanza wiki hii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news