DAR-Ubalozi wa India nchini Tanzania umekutana na kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa lengo la kupata taarifa zaidi kuhusu zoezi la kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia linalotarajiwa kufanyika Tanzania Bara mwaka huu.
Mazungumzo hayo yamefanyika Mei 14, 2024 katika Ofisi za PURA jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu wa Pili wa Balozi wa India nchini Tanzania (Masuala ya Biashara),Bw. Narender Kumar na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Danstan Asanga.
Akizungumza katika kikao kati ya pande hizo, Bw. Kumar alieleza kuwa, mara baada ya kusikia mpango wa Serikali wa kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia kupitia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati mwaka 2024/25, Ubalozi wa India Nchini Tanzania uliona vyema kukutana na Mamlaka husika kufahamu kwa mapana kuhusu suala hilo ili waweze kutoa taarifa kamili kwa kampuni na wadau nchini India.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo