Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 17,2024

SHINYANGA-Umoja wa Mawakala wa Kituo kidogo cha mabasi kilichopo Kata ya Majengo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wamelazimika kuchangisha fedha kila mmoja ili kupata shilingi milioni moja ya kumchukulia fomu ya kugombea urais, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kukoshwa na utendaji kazi wake.
Mwenyekiti wa umoja huo, Baraka Jilumbi amebanisha hayo Mei 16,2024 wakati wa hafla ya ufunguzi wa shina la wakereketwa kituoni hapo, ambapo amesema, awali walikuwa wakionekana wahuni kwenye jamii inayowazunguka,lakini baada ya kuweka utaratibu wa kutambuliwa kisheria wamewiwa kumchukulia fomu ya kugombea Rais Dkt. Samia.











Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news