Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 19,2024

ARUSHA-Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha kuanza uchunguzi dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Mhandisi Juma Hamsini na baadhi ya wasaidizi wake kutokana na kukabiliwa na tuhuma za rushwa na upigaji wa fedha za walipa kodi.
Ameyasema hayo Mei 18,2024 wakati akizungumza na wadau wa utalii mkoani hunk, ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Mussa kuwasimamisha kazi watumishi wote waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo ili kupisha uchunguzi.

RC Makonda amechukua hatua hizo baada ya Mwenyekiti wa Waongoza Watalii Mkoa wa Arusha,Wilbard John Chambulo kudai kuwa, baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha wamekuwa wakitengeneza nyaraka bandia pamoja na kuchepusha baadhi ya makusanyo ya kodi zinazotokana na Sekta ya Utalii.

Amemuambia mkuu wa mkoa kwamba, watumishi hao wamekuwa na makampuni hewa ya utalii pamoja na kuwa na namba tofauti za ulipaji wa kodi na usajili hewa wa makampuni yenye kufanana na makampuni halisi ya utalii yalipo ndani ya jiji hilo.








Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news