DAR-Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeonya baadhi ya watu wasio waadilifu kuacha vitendo vya kitapeli na kuwalaghai Watanzania kutoa fedha ili kujiunga na mafunzo, kwani mafunzo hayo yanatolewa bure.
Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye ni Mkuu wa Tawi la Utawala JKT ameyasema hayo Mei 24,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wito wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria Mwaka 2024.
Ni vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2024 kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ili kujengewa uzalendo, umoja na stadi za maisha.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo