Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 31,2024

DODOMA-Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya shilingi 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara hapa nchini.
Mheshimiwa Kirumba ameshauri hilo Mei 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.
“Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya.

"Tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema, laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini shilingi 50 ili iweze kuisaidia Road Fund, na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund,"amesisitiza Mheshimiwa Santiel.






















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news