DAR-Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeingia makubaliano ya kupeleka marubani wake kufundisha na kusimamia ndege mpya za Airbus A220 za Kampuni ya Ndege ya Ibom Air inayomilikiwa na Jimbo la Akwa Ibom nchini Nigeria.
Ni baada ya ATCL kuonesha uzoefu wa muda mrefu wa kumiliki ndege za Airbus A220-300 na pia kuridhishwa na kiwango cha umahiri wa marubani wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi, amethibitisha kuwepo kwa makubaliano hayo ambapo amesema,ATCL imetoa marubani wake waandamizi wawili ambao watakuwa na jukumu la kuwafundisha kwa vitendo marubani na walimu wa marubani wa Ibom Air kwa muda wa miezi sita.
“Marubani wa ATCL watakuwa na jukumu la kufundisha na kusimamia mafunzo kwa vitendo hadi watakapojiridhisha kuwa marubani wanafunzi na walimu wao wamefikia viwango vinavyotakiwa kurusha ndege hizo ambapo Kampuni ya Ibom Air itailipa ATCL gharama za mafunzo hayo kwa mujibu wa mkataba kwa kipindi chote cha makubaliano.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo