Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 18,2024

TANGA-Dereva wa pikipiki ya Afisa Mifugo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Abel Adamson Mwaipopo (25) amefariki dunia baada kumgonga ndege aina ya bundi na kisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na kuanguka, hivyo kusababisha kifo.  Albert Msando ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni amesema tukio hilo limetokea Mei 17,2024 eneo la Sindeni jirani na kona ya PRS ambapo dereva huyo alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili STM 0232 .

"Kwanza naomba nitolee ufafanuzi jambo hili,kwani aliyefariki sio Afisa Mifugo kama wengi walivyosema kwani Afisa Mifugo wetu wa wilaya ni mwanamke na aliyefariki ni mwanaume dereva ambaye anamwendesha Afisa Mifugo.

“Ajali ni kama ajali nyingine, lakini akishahusishwa bundi mara zote tayari kunakuwa na hizo imani za kishirikina na hofu kwa watu kwamba amegonga bundi kafa na yeye mwenye amekufa, lakini vilevile inawezekana kwa kiasi kikubwa labda alivyomuona bundi katika kujaribu kumkwepa hakuchukua tahadhari akapata ajali.

"Ni uwezekano vilevile hakuwa amevaa kofia ngumu, hivyo katika kuanguka akajigonga akapata madhara akafariki, hivyo inawezekana ikawa ni ajali ya kawaida,lakini kwa sababu imemuhusisha bundi lazima italeta taharuki kuwa inahusiana na mambo ya kishirikina,”amefafanua.






Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news