Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 28,2024

PWANI-Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, David Mramba amesema,taasisi na mashirika yanayoanzishwa kuisemea Serikali na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yanatakiwa kuhakikisha hayatumiki kama kichaka cha uhalifu.
Ametoa rai hiyo mwishoni mwa wiki alipoyakutanisha mashirika yasio ya kiserikali na taasisi zenye mrengo mmoja wa kuisemea Serikali na chama zinazofanya kazi zake mkoani hapa.

Mramba amesema, yapo baadhi ya mashirika yamegeuka kichaka cha kuhifadhi maovu, kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya uanzishwaji na kuchafua Serikali na chama tawala jambo ambalo halipendezi na halikubaliki nchini.













Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news