Hii hapa, orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya kati 2024

DODOMA-Wanafunzi 188,787 waliokidhi vigezo wakiwemo wenye mahitaji maalumu 812 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali za sekondari vikiwemo vyuo vya kati kwa mwaka 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 30,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma.

"Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tumekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya ufundi vya Serikali kwa mwaka 2024 ambapo wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali, zisizo za Serikali na watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

“Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule, hivyo hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule kutokana na ukosefu wa nafasi."


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news