Huduma mpya 16 za Ubingwa Bobezi zimeanzishwa nchini

DODOMA-Kutokana na uwekezaji wa kimkakati uliofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, imeanzisha huduma mpya 16 za ubingwa bobezi nchini. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo bungeni Mei 13, 2024 akiwa anawasilisha hotuba yake ya bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2024/25 akielezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika utoaji wa huduma za Kinga nchini.

"Huduma hizo zinajumuisha kutenganisha mapacha walioungana kwa kutumia watalam wa ndani, tiba hewa mgandamizo, upasuaji kwa njia ya matundu madogo, kutoa kizazi, upasuaji kwa watu wenye shida ya kumeza chakula, upasuaji rekebishi wa vipara,"mesema Waziri Ummy.

Amesema, huduma nyingine ni pamoja na upasuaji wa kupunguza mfuko wa chakula kwa wagonjwa wenye uzito uliopitiliza pamoja na kufungua mishipa ya miguuni iliyoziba kwa kuweka 'stent' kwenye mishipa mikubwa ya damu iliyopasuka.

Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara inaeendelea kutekeleza mpango wa huduma za Mkoba za Kibingwa katika ngazi ya Halmashauri zote 184 na vituo vya afya 72 ambapo seti ya Madaktari Bingwa wa fani Tano wanashiriki katika kila Hospitali ya halmashauri kutoa huduma za kibingwa na kujenga uwezo wa wataalam katika ngazi ya halmashauri.

"Nitoe rai kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi pindi huduma hizi zinaposogezwa karibu na maeneo yao, ninawaahidi kuwa mpango huu utaendelea mpaka tutakapokamilisha Mikoa yote na Halmashauri zote,"amesema Waziri Ummy.

Vilevile, Waziri Ummy ameswma Wizara imewezesha Hospitali za Rufaa za Mikoa Nane kutoa huduma za kibingwa katika fani Nane ikilinganishwa na Hospitali za Rufaa za Mikoa Mitano kwa kipindi kama hicho mwaka 2022/23.

Aidha, Waziri Ummy amebainisha kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 5,000,000,000 kimetolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia matibabu kwa wagonjwa 237 wasio na uwezo wa matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news