Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, Makamu wa Rais atoa neno

DAR-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa wito kwa Watanzania kuhakikisha matumizi adili ya rasilimali za nchi kama njia ya kumshukuru Mungu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap iliyofanyika katika viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2024.

Makamu wa Rais ametoa wito huo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (OFMCap) iliyofanyika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima – Msimbazi Centre Dar es Salaam.

Amesema Viongozi na Watumishi wa serikali wanayo nafasi kubwa ya kusimamia matumizi ya rasilimali za nchi na kuwaongoza watanzania katika ni kuhakikisha mazingira mazuri ya nchi yanatunzwa na kurekebishwa pale ambapo tayari yameharibiwa kwa uchomaji moto hovyo wa misitu, uharibifu wa vyanzo vya maji, uchafunzi wa mazingira ya mito na bahari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap iliyofanyika katika viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakimkabidhi zawadi ya kifaa muhimu cha Ibada (Monstrance) kinachotumika katika kuabudu Sakramenti Takatifu ya Ekaristi na Baraka Kuu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (OFMCap) mara baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake iliyofanyika katika viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2024.

Amesema ni vema kumshukuru Mungu kwa neema zake kwa kusali au kumtolea maombi ya shukurani pamoja na kutimiza wajibu wa kutunza na kustawisha fadhila zote ambazo Mungu ametutendea. Amesema Watanzania wanaweza kumshukuru Mwenyezi Mungu vizuri zaidi kwa kuthamini na kuitunza nchi nzuri ya Tanzania tuliyojaaliwa.

Amewasihi Watanzania kuwajibika kumshukuru Mungu kwa amani na mtangamano katika Taifa kwa miaka 63 ya uhuru na kuwezesha kuishi kwa ushirikiano baina ya watu wa imani, rangi, kabila na itikadi za kisiasa tofauti tofauti. Amesema ni baraka za kushukuru kwa kuwa na Taifa lenye ardhi nzuri, maziwa, mito na vijito, bahari, misitu, mabonde na milima, madini ya aina mbalimbali, wanyama wa kufugwa na wa porini, ndege, wadudu, neema ya mvua na hali ya hewa nzuri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Viongozi wa Kanisa pamoja na Waumini mbalimbali mara baada ya kukamilika kwa Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (OFMCap) iliyofanyika katika viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2024.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi mara baada ya kukamilika kwa Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap katika viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap mara baada ya kumalizika kwa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap iliyofanyika katika viwanja vya Msimbazi Centre Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tarehe 16 Mei 2024.

Makamu wa Rais amesema ni wajibu kushukuru kwa kuwa shukurani inafungua milango iliyofungwa hususan pale binadamu anapokabiliwa na ugumu wa maisha, magonjwa, biashara kudorora, changamoto za kazi na mara zote Mungu humpa anayeshukuru zaidi ya kile anachoshukuru kukipokea kwani shukurani inaonesha kwamba mtoa shukurani anatambua mchango wa mwenyezi Mungu katika maisha yake.

Makamu wa Rais amempongeza Askofu Mkuu Jude Ruwa’ichi kwa kutimiza miaka 25 ya Uaskofu na kukumbuka kumshukuru Mwenyezi Mungu, ambaye amemjalia neema nyingi na kumwezesha kutekeleza utume wake kikamilifu kwa miaka yote 43 ya Upadre wako ambayo 25 amekuwa Askofu. 

Aidha amempongeza kwa mchango mkubwa katika kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) na Vyuo Vikuu Vishiriki vya Mtwara, Songea na Moshi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news