Kamati yasisitiza uharaka wa mageti janja ya kukatia tiketi

DAR-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa rai kwa Serikali kuhakikisha wanaweka mageti janja kwenye vituo vya kukatia tiketi ili kuongeza mapato na kuboresha huduma kwa Watanzania.
Rai hiyo imetolewa leo Mei 4, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,  Mhe. Justine Lazaro Nyamoga alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara ya kikazi kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka na ujenzi wa Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Amesema,haiwezekani kuona wananchi mpaka sasa bado wanapanga foleni kukata tiketi wakati mageti janja yameletwa na serikali,lakini hajafungwa na jambo hilo linawakera wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Ameendelea kufafanua kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha inakusanya mapato kwa kutumia mifumo ya TEHAMA na kuwapunguzia adha wananchi ya kupanga foleni kusubiri huduma.

"Inashangaza kuona mpaka sasa wananchi wanapanga foleni kukata tiketi wakati katika kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ilikuwa inatakiwa wananchi kuwa na kadi maalum za huduma ya usafirishaji,"amesisitiza Mhe Nyamoga

Amesema, si vizuri kuwaacha wananchi wanapanga foleni kukata tiketi ambapo wanatumia muda mrefu ambapo kama serikali ni jukubu let kuhakikisha tunwarahisishia huduma wananchi.

Aidha, wameipongeza Serikali kwa kuhakikisha wanatumia wataalam wa ndani katika kuujenga mfumo wa matumizi ya mageti janja ambao utasaidia kupunguza mianya ya rushwa na kuongeza mapato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news