Kamati yataka mwendokasi yafike hadi Mbagala Kijichi

DAR-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Lazaro Kamoga imefanya ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundombinu na uendeshaji wa mabasi yaendayo haraka.
Akiongea na wananchi wa eneo la Mbagala Kijichi, Mhe.Nyamoga ameitaka serikali kuhakikisha wanapeleka huduma ya mabasi katika eneo la Mbagala Kijichi ili waweze kupata huduma bora za usafiri katika eneo hilo.

"Wananchi wa Mbagala wanahitaji huduma ya mabasi yaendayo kwa haraka kutokana na wingi wa wananchi pamoja na uhitaji wa huduma hiyo, hivyo ninaiomba Serikali iweze kutoa huduma hiyo kwa haraka," amesisitiza Nyamoga.
Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Zainab Katimba amesema, tayari mradi umekamilika kwa asilimia 98 hivyo itaanza kutoa huduma ya usafiri katika eneo hilo.
"Mradi umekamilika kwa asilimia 98 hivyo tupo tayari kuanza kutoa huduma ya mabasi yaendayo kwa haraka katika eneo hili ila tunakamilisha asilimia zilizobaki," amesema Mhe.Katimba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news