Maafisa Ushirika mbaroni kwa ulanguzi wa tumbaku Sikonge

TABORA-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Sikonge mkoani Tabora kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Tabora imewafikisha mahakamani washtakiwa wawili ambao ni Emmanuel Ado Hyera na Michael Emmanuel Ngusa.
Hatua hiyo imechukuliwa Mei 24,2024 ambapo washtakiwa hao ni Maafisa Ushirika wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Kwa pamoja maafisa hao wamefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Na. (ECO:13092/2024) ambapo wanatuhumiwa kufanya biashara haramu ya kulangua tumbaku bila kuwa na leseni.

Kesi imesomwa mbele ya Mheshimiwa Ngaeje (SRM) ambapo washtakiwa wote wawili wanashtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha PCCA (sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022).

Ilidaiwa kwamba, maafisa hao walitumia mamlaka yao kufanya biashara haramu ya kulangua tumbaku bila kuwa na leseni kinyume na kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Tobacco Industry Act ya Mwaka 2001 na kujipatia faida.

Aidha,Jamhuri imewasilisha maombi ya kuzuia mali za washtakiwa kwa kuwa zinahusiana moja kwa moja na makosa yao.

Washtakiwa wote wamekana mashtaka yao na wameachiwa kwa dhamana.

Kesi itatajwa tena Mei 27, 2024 kwa kutaja hoja za awali na Mei 28, 2024 kwa ajili ya kupata uamuzi mdogo wa maombi ya zuio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news