Madereva watatu wakamatwa kidigitali kwa mwendokasi

ARUSHA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linaendelea kutumia mifumo ya TEHAMA katika kudhibiti makosa ya usalama barabarani ambapo kupitia mfumo huo leo Mei 27,2024 majira ya alfajiri limewabaini madereva watatu ambao wamevunja sheria za usalama barabarani.
Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Zauda Mohamed amesema kuwa,kikosi hicho kinaendela kuboresha mifumo yake ambapo kwa sasa kitumia mfumo wa kufuatilia magari (VTS) katika kuwabaini madereva wanao wanaendesha magari mwendokasi.

SSP Zauda ameongeza kuwa, kikosi hicho kinaendelea kutumia mifumo hiyo ili kuondoa malalamiko kwa watumiaji wa vyombo na wananchi kuhusiana na madereva wanavunja sheria za usalama barabarani huku akiweka wazi kuwa mapema leo tayari wamekamata madereva watatu waliozisha mwendo.
Aidha, amesema kuwa kupitia mfumo huo umewasaidia katika kufuatilia madereva wakiwa maeneo tofauti tofauti ambapo alibainisha kuwa idadi kubwa ya madereva wanatumia vyombo vya moto hususani magari ya abiria wameendelea utii wa sheria bila shuruti huku akiwasihi kuwa kikosi hicho kinaendelea kuwafuatilia madereva wanao kikuka sheria kupitia mifumo hiyo.

Sambamba na hilo amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na wamiliki kuendelea kufanya marekebisho ya vyombo vyao kutokana na ongezo la abiria wengi hasa kipindi hiki ambacho wanafunzi wengi wamefunga shule kwa ajili ya mapumziko.
Kwa upande wake Apolinary Mwacha ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mabasi Mkoa wa Arusha licha ya kushukuru kupata nafasi ya kuona mfumo unavyofanya kazi amesema kuwa, utasaidia kupunguza mgongano baina ya askari na madereva huku akiwaomba madereva wenzake kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news