Magari ya abiria yaliyokwama siku sita barabara ya Lindi-Dar yaanza safari

LINDI-Magari ya mizigo, mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama kwa siku sita katika barabara ya Lindi hadi Dar es Salaam eneo la Njia Nne (Mikereng’ende) hadi Somanga yakitokea Lindi kuelekea Dar es Salaam yameanza kuruhusiwa kuendelea na safari.
Hatua hiyo imechukuliwa leo asubuhi Mei 9, 2024 mkoani Lindi mara baada ya kukamilisha urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo ya Mikereng’ende, Songas na Somanga ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.
Akisimamia zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amewataka wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara kusafiri kwa tahadhari ambapo maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.

“Naipongeza Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zilizofanyika ndani ya muda mchache na leo tunashuhudia magari yaliyokwama yameruhusiwa kuendelea na safari,”amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, kazi ya urejeshaji wa miundombini ya barabara ya Lindi - Dar es Salaam eneo la Nangurukuru ipo katika hatua ya ukamilishaji chini ya usimamizi wa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara (TANROADS).
Kwa upande wa wananchi, wameishukuru Serikali kwa namna ambavyo wamerejesha mawasiliano ya barabara kwa vipande hivyo na kuweza kuruhusiwa leo baada ya siku sita kukwama katika barabara hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news