LONDON-Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amewasilisha mada juu ya mageuzi ya Elimu Tanzania na kuwakosha wajumbe wa Mkutano wa Elimu Duniani unaofanyika jijini London, Uingereza.
Tanzania inashiriki katika mkutano huo ulioleta pamoja nchi zaidi ya 200 duniani kujadili maendeleo ya elimu duniani ikiwa ni nguzo kuu ya kuandaa rasilimali watu wenye ujuzi na mtaji mkubwa katika kuleta maendeleo.
Katika wasilisho, Prof. Mkenda ameelezea namna Tanzania ilivyoanza kazi ya utekelezaji mageuzi kwa kufanya mitaala kulenga elimu ujuzi na kusisitiza umuhimu wa wadau wa elimu wakajielekeza katika kutatua changamoto kimfumo ikiwemo ugharamiaji, vifaa, walimu bora na ujuzi.