Majaji, mahakimu wanawake Tanzania kushiriki Mkutano wa IAWJ nchini Ghana

NA MARY GWERA
Mahakama Accra

MAJAJI na Mahakimu Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wanatarajia kuungana na Majaji wanawake wenzao kutoka Ukanda wa Afrika kushiriki katika Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (IAWJ) utakaofanyika jijini Accra nchini Ghana.
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Barke Sehel.

Akizungumza katika mahojiano maalum leo tarehe 12 Mei, 2024, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Barke Sehel amesema kuwa, Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi kesho tarehe 13 hadi 18, Mei, 2024 na utafunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. Nana Addo Dankwa Akufo-Addo.

“Mkutano huu ni wa Kikanda kwa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake, Mkutano huu unakutanisha wanachama Majaji na Mahakimu wanawake Afrika kwa ujumla. Kwa upande wa Tanzania tutakaoshiriki katika Mkutano huo ni 18 na idadi hii imejumuisha na wenzetu wa Zanzibar,” amesema Mhe. Sehel.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kutoka jijini Accra Ghana leo tarehe 12 Mei, 2024.

Mwenyekiti huyo ameeleza kwamba, katika Mkutano huo, Mahakama ya Tanzania itapata nafasi ya kutoa mada ya kuelezea hatua zinazochukuliwa na TAWJA katika kumpa nafasi mwanamke kwenye Uongozi hasa kwenye Mahakama.

Kaulimbiu ya Mkutano huo inasema ‘Nafasi ya Majaji Wanawake katika kupambana na mila potofu katika ulimwengu wa sasa.’Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Barke Sehel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wanachama wa TAWJA walipowasili jijini Accra leo tarehe 12 Mei, 2024 maalum kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (IAWJ) Ukanda wa Afrika utakaoanza kufanyika kesho tarehe 13 Mei, 2024. Kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Monica Otaru.

Mbali na TAWJA, Vyama vingine vitakavyoshiriki katika mkutano huo ni kutoka Nigeria, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Cote d’Ivoire na nyingine.

Kiongozi wa msafara wa wanachama wa TAWJA, Mhe. Sehel pamoja na wenzake wamewasili leo hii jijini Accra majira ya saa 5 asubuhi tayari kwa kushiriki kikamilifu mkutano huo muhimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news