Makamu wa Rais awaachia ujumbe wahandisi washauri

DAR-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema, upo umuhimu wa kupitia upya vipengele katika nyaraka zinazoandaliwa na Taasisi ya Kidunia ya Mikataba ya Ujenzi na Ununuzi (FIDIC) ili kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji katika makosa na madhaifu ya wahandisi washauri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA),Mhandisi Falles Ngeleja juu ya kuongeza ubunifu katika ujenzi wa barabara vijijini ili ziweze kudumu zaidi, ametoa amelekezo hayo wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam leo Mei 27,2024.

Makamu wa Rais amesema hayo leo Mei 27,2024 wakati akifungua Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Rais wa Umoja wa Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Chedi Masambaji wakati alipowasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam kwaajili ya Ufunguzi wa Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya tuzo Rais wa Umoja wa Wahandisi Washauri Afrika, Mhandisi Abe Thele mara baada ya kufungua Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam leo.

Amesema yapo mapungufu yanayosababisha uzembe na kushindwa kukamilisha miradi kwa ubora na muda uliopangwa na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa mteja ikiwa ni pamoja na Serikali.
Aidha Makamu wa Rais amesema ni wakati sasa, uandaaji wa nyaraka za mikataba ya ujenzi na ununuzi za FIDIC kuweka kipaumbele matumizi ya wazawa katika miradi husika ili kukuza wahandisi washauri wa ndani kujiongezea maarifa ya kiteknolojia na uzoefu.

Amesema, wahandisi washauri wa ndani wanakabiliwa na ukosefu wa ufadhili ikiwemo katika tafiti na maendeleo pamoja na ukosefu wa vifaa vya kisasa tofauti na wahandisi washauri wa kigeni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco) juu ya kuongeza ubunifu katika kushughulikia changamoto za usafirishaji na usambazaji umeme nchini. Ametoa amelekezo hayo wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam leo.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema kuna tofauti kubwa katika ubora wa ushauri wa uhandisi na elimu ya ufundi shirikishi kote barani Afrika ambayo ubora wake mara nyingi haukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Amesema,jambo hilo linasababisha ugumu katika kubakiza wahandisi washauri wenye talanta barani Afrika ambapo Idadi kubwa ya wahandisi washauri wa juu wamehama bara hilo ili kutafuta fursa zaidi nje ya Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais amewaasa kutumia mkutano huo kutambua umuhimu wa vituo vya ubunifu katika nchi nyingi za Afrika kama jukwaa la wahandisi washauri kushirikiana na kubadilishana mawazo ya kibunifu ili kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika mataifa husika.

Kwa upande wake Prof. Patrick Lumumba ambaye ni mtoa mada katika mkutano huo ametoa rai kwa Wahandisi barani Afrika kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu ya Bara hili ili lengo la ufanyaji biashara baina ya mataifa ikiwemo kutumia Ukanda huru wa Biashara Barani Afrika (AfCFTA) liweze kutimia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wahandisi Washauri Afrika mara baada ya kufungua Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam leo.

Amesema,miundombinu barani Afrika imeendelea kuwa changamoto inayokwamisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazorudisha nyuma maono yaliyokuwepo wakati wa uanzishwaji wa mataifa mengi barani Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Prof. Patrick Lumumba ambaye ni mtoa mada katika Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam mara baada ya kufungua mkutano huo leo.

Pia, Prof. Lumumba amesema,bado mataifa mengi yameendelea kutumia wahandisi wa kigeni licha ya mataifa hayo kuwa na wahandisi wazawa waliopata elimu ya katika vyuo vikuu mbalimbali.

Ametoa wito kwa vyuo vya elimu ya juu barani Afrika kuwekeza katika tafiti zitakazosaidia upatikanaji wa nishati kama vile nishati ya jua na nishati ya upepo ili Mataifa yenyewe ya Afrika yaweze kujitegemea katika kuzalisha na kusambaza nishati hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news