ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameishukuru wadau wa maendeleo wa Korea kupitia Jumuiya ya Lady Fatima Charity kwa msaada wa dola za kimarekani 37,000 kwa ajili kuwezesha upatikanaji wa kutoa Taulo za kike (Tumaini Kits) zinazotengenezwa na ZMBF na zimenufaisha zaidi ya Wasichana 2,500 wa shule za Pemba.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo Mei 11,2024 alipokutana na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya kudumu ya Bunge la Korea , Mhe.Sul Hoon na ujumbe wake waliofika ofisini kwake Ikulu Migombani.
Mama Mariam Mwinyi amesema, ndoto yake ni kuwasaidia kuwainua kiuchumi Wanawake hususani wakulima wa Mwani kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kuchakata zao hilo , na amewakaribisha Serikali ya Korea katika kuendeleza ushirikiano na kujifunza zaidi kutoka kwao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Kudumu ya Bunge la Korea, Mhe.Sul Hoon na ujumbe wake wameahidi kushirikiana na Taasisi ya ZMBF katika nyanja mbalimbali hususani vipaumbele vya taasisi hiyo.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Mama Mariam Mwinyi
Mariam Mwinyi
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)