Manchester United yatwaa Kombe la FA England

LONDON- Manchester United imetwaa Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya waliokuwa wanashikilia taji hilo, Manchester City.
Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao umepigwa Mei 25,2024 katika dimba la Wembley lililopo London, Uingereza.

Pengine, Manchester United wamelipa kisasi cha fainali ya mwaka jana ambayo Manchester City walishinda mabao 2-1.Alejandro Garnacho Ferreyra alilipa bili kwa waajiri wake baada ya dakika ya 30 kufunga bao la kwanza.

Dakika tisa baadaye, Kobbie Boateng Mainoo aliongeza bao la pili ambalo liliwafanya Manchester United kwenda mapumziko wakiwa vema.

Hata hivyo, kipindi cha pili hakikuwa riziki kwao, kwani ilikuwa bahati ya Manchester City baada ya Jérémy Baffour Doku dakika ya 87 kufunga hesabu kwa bao la kufutia machozi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news