Maswali yazidi kuwa mengi kifo cha Rais Ebrahim Raisi wa Iran, msimamo wake umemponza?

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ebrahim Raisi mwenye umri wa miaka 63, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi,Hossein Amir-Abdollahian (60) wakiwemo maafisa wa Jamhuri hiyo wamefariki katika ajali ya helikopta.
Watu wakifuatilia habari za kuanguka kwa helikopta iliyombeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi kwenye runinga katika duka moja mjini Tehran mnamo Mei 19, 2024.(Picha na WANA/Reuters).

Ebrahim Raisi na Amir-Abdollahian walikuwa katika ziara ya mpaka wa Azerbaijan wakati helikopta yao ilipoanguka katika eneo la milimani Kaskazini-Magharibi mwa Iran mnamo Mei 19,2024 na kuwaua wote waliokuwa ndani.

Ajali hiyo inakuja wakati eneo la Mashariki ya Kati likiwa halijatulia kutokana na vita vya Israel na Hamas, ambapo Raisi chini ya Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei alianzisha shambulio la kipekee la ndege na kombora dhidi ya Israel mwezi uliopita.

Chini ya Raisi, Iran ilirutubisha madini ya uranium kuliko hapo awali kwa viwango vya kiwango cha silaha, na hivyo kuzidisha mivutano na nchi za Magharibi huku Tehran pia ikisambaza ndege zisizo na rubani za mabomu kwa Urusi kwa vita vyake nchini Ukraine na vikundi vya wanamgambo wenye silaha kote katika kanda hiyo.

Wakati huo huo, Iran imekabiliwa na maandamano makubwa ya miaka mingi dhidi ya demokrasia ya Shiite juu ya uchumi wake mbaya na haki za wanawake na kufanya wakati huo kuwa nyeti zaidi kwa Tehran na mustakabali wa nchi.

Runinga ya taifa haikutoa sababu za haraka za ajali hiyo huko Azerbaijan Mashariki mwa Iran, ingawa ilitaja tukio hilo kama kutua kugumu kulitokea karibu na Jolfa, mji ulio kwenye mpaka na taifa la Azerbaijan, takriban kilomita 600 (maili 375) Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa Iran, Tehran.

Afisa mmoja wa serikali katika eneo hilo alitumia neno “kuanguka,” lakini wengine walirejelea ama “kutua kwa shida” au “tukio.”

Mapema Jumatatu asubuhi, mamlaka ya Uturuki ilitoa kile walichokitaja kuwa picha za ndege zisizo na rubani zinazoonesha kile kilichoonekana kuwa moto nyikani ambao walidhania kuwa mabaki ya helikopta.

Viratibu vilivyoorodheshwa kwenye picha viliweka moto huo umbali wa kilomita 20 Kusini mwa mpaka wa Azerbaijan na Iran kwenye kando ya mlima mkubwa.

Kanda za video zilizotolewa na IRNA mapema Jumatatu zilionesha kile ambacho shirika hilo lilieleza kama eneo la ajali, katika bonde lenye mwinuko katika safu ya milima ya kijani kibichi.

Aidha,wanajeshi waliokuwa wakizungumza katika lugha ya Kiazeri walisema, “Haya, tumeipata.”

Muda mfupi baadaye, runinga ya Serikali katika maandishi kwenye skrini ilieleza "Hakuna dalili ya moja kwa moja kutoka kwa watu waliokuwemo."

Haikufafanua zaidi, lakini shirika la habari la Tasnim lilionesha waokoaji wakitumia ndege ndogo isiyo na rubani kuruka juu huku wakiteta wenye kwa wenyewe.

Viongozi wa kidini walikuwa wamewahimiza wananchi kusali. Televisheni ya Taifa ilirusha picha za mamia ya waumini, wengine wakiwa wamenyoosha mikono katika dua, wakisali katika Madhabahu ya Imam Reza katika mji wa Mashhad, mojawapo ya maeneo takatifu zaidi ya Uislamu wa Shiite, na pia huko Qom na maeneo mengine kote nchini humo.

Runinga ya Taifa ilipeperusha maombi hayo bila kukoma. Huko Tehran, kundi la wanaume waliopiga magoti kando ya barabara walifunga nyuzi za shanga za maombi na kutazama video ya Raisi akiomba, baadhi yao wakilia.

"Ikiwa chochote kitampata tutavunjika moyo," mmoja wa wanaume hao, Mehdi Seyedi alisema. "Maombi yafanye kazi na arudi kwenye mikono ya taifa akiwa salama na mzima."(NA)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news