Mauricio Pochettino aondoka Chelsea

ENGLAND-Mauricio Pochettino ameondoka Chelsea baada ya kuifundisha kwa msimu mmoja tu kwa makubaliano, klabu hiyo ya Uingereza imethibitisha Jumanne.
Pìcha na Football.London

The Blues walimaliza katika nafasi ya sita kwenye Premier League kutokana na mwenendo mzuri kuelekea mwisho wa msimu.

Aidha, kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 aliwasili London Magharibi akiwa na jukumu la kuirejesha Chelsea kwenye mstari baada ya kumaliza nafasi ya 12 katika msimu wa Ligi Kuu ya 2022/23.

Ni kutoka chini ya meneja wa muda wa Chelsea, Frank Lampard.

Ingawa Chelsea walianza msimu vibaya na kujikuta wakiwa nyuma ya ligi licha ya kutumia pesa nyingi kuliko klabu yoyote barani Ulaya, Pochettino alifanikiwa kuipandisha klabu hiyo ya London hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Pia, alifanikisha klabu yake kutinga fainali za Kombe la Ligi ya Uingereza pamoja na nusu fainali ya Kombe la FA chini ya uongozi wake.

"Chelsea FC inathibitisha kwamba klabu na Mauricio Pochettino wamekubaliana kuachana," Chelsea ilieleza katika taarifa.

Katika kipindi cha miaka miwili tu chini ya umiliki wa muungano wa Marekani unaoongozwa na mmiliki mwenza wa LA Dodgers Todd Boehly na Clearlake Capital, Chelsea wametumia zaidi ya pauni bilioni 1 (dola bilioni 1.3) kununua wachezaji wapya.

Aidha, sehemu kubwa ya hizo fedha ilitumika kwa nyota wanaochipukia ili kuendelea kuimarisha safu ya klabu hiyo.

Pochettino ni meneja wa nne kuondoka chini ya utawala wa Boehly baada ya Thomas Tuchel, Graham Potter na Frank Lampard.

Kwa mujibu wa Daily Telegraph, Pochettino alikutana na Boehly kwa chakula cha jioni Ijumaa kabla ya kuondoka kwake kuthibitishwa baada ya ukaguzi wa mwisho wa msimu.

Alikopita Mauricio Pochettino;

Club & rolefrom / untilGames / PPG
Chelsea FC23/24 (Jul 1, 2023) /
23/24 (May 21, 2024)
51 / 1.78
Paris Saint-Germain20/21 (Jan 2, 2021) /
22/23 (Jul 5, 2022)
84 / 2.15
Tottenham Hotspur14/15 (Jul 1, 2014) /
19/20 (Nov 19, 2019)
293 / 1.84
Southampton FC12/13 (Jan 18, 2013) /
13/14 (Jun 30, 2014)
60 / 1.45
RCD Espanyol Barcelona08/09 (Jan 20, 2009) /
12/13 (Nov 26, 2012)
161 / 1.22
Women's football08/09 (Dec 1, 2008) /
08/09 (Jan 1, 2009)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news