Mheshimiwa Ulega awafariji waathirika wa mafuriko Mkuranga

PWANI-Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewatembelea na kuwafariji wananchi waliothiriwa na mafuriko katika Kata za Kisiju na Shungubweni wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akitoa salamu za pole Mei 1, 2024, Mhe. Ulega amesema kuwa Mhe. Rais Samia amemtuma kuwafikishia wananchi hao salamu zake za pole pamoja na chakula, magodoro na vifaa vingine vya ndani ili viwasaidie katika kipindi hiki wakati serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi hao wanarejea katika maisha yao ya kawaida.

Sehemu kubwa ya wananchi hao ambao Mhe. Ulega amewatembelea nyumba zao zimeathiriwa kwa kuzingirwa na maji na kupelekea kukosa makazi na hivyo kulazimika kukaa katika makambi.
Jumla ya vitu ambavyo Mbunge huyo amekabidhi kwa niaba ya Mhe. Rais Samia ni Mchele tani 4, Unga tani 5 na Maharagwe tani 10 ambavyo amekabidhi kwa Vijiji vya Kerekese,Kalole,Mavunja na Kisiju pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news