Miradi ya shilingi bilioni 40.9 yafikiwa na Mwenge wa Uhuru wilayani Ilala

DAR-Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 katika Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam umekimbizwa umbali wa kilomita 81.7 na kupitia miradi saba yenye thamani ya shilingi 40,941,764,931.
Mwenge wa Uhuru kaka wilaya hiyo ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Eliakimu Mnzava umetembelea, umekagua, umeweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Aidha,miradi ambayo imepitiwa na Mwenge huo ni ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo 45 Shule ya Sekondari Minazi mirefu, Kituo cha Polisi Mwanagati.

Pia, Kituo cha Afya Kinyerezi, Kituo cha kutengeneza mapambo ya Gypsum Good Hope Segerea, Barabara ya Tukuyu kilomita 0.62 kwa kiwango cha lami, na mradi wa utoaji elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Alimuntazir.
Miradi yote iliyopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ilala imepitishwa na Mwange huo hakuna mradi uliokataliwa.

Sanjari na hilo katika maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru umepita umeendelea kuelimisha wananchi juu ya Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe pamoja na Rushwa.
Leo Mei 9, 2024 Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zinaendelea kukimbizwa Katika Wilaya ya Temeke.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news