TANGA-Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Dkt. Erasmus Kipesha leo Mei 27, 2024 amehudhurua ufunguzi wa maadhimisho ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu katika viwanja vya shule ya sekondari Popatlal jijini Tanga.

Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ya wiki moja ni Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda hilo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi wa TEA, Bw. Masozi Nyirenda.


Maadhimisho haya yenye kauli mbiu ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi shindani yameanza Mei 25 na tamati rasmi itakuwa Mei 31, 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha na Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi,Bw. Masozi Nyirenda wakifurahia jambo katika banda la TEA, kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal, Jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Umma, Bi. Bestina Magutu.


Awali, Dkt. Kipesha alitembelea banda la Mamlaka katika viwanja hivyo na kukutana baadhi ya wanufaika wa mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) uliosimamiwa na TEA wakiwa na bidhaa zao wanazozalisha baada ya kupatiwa mafunzo.