Muhimbili yajiwekea mkakati maalum kutoa huduma kwa Wacomoro

DAR-Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Prof Mohamed Janabi amesema kuwa, wana mkakati maalum wa kutoa huduma za tiba kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutoka visiwa vya Comoro kutokana na ongezeko la idadi yao katika siku za karibuni.
Prof.Janabi amesema hayo alipokuwa akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu aliyefika kumuaga.

Prof.Janabi ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Utalii wa Matibabu alieleza kuwa kwa hivi sasa wana mratibu maalum wa wagonjwa toka nje ya nchi na pia mkalimani wa lugha ya Kifaransa ili kurahisisha mapokezi ya wagonjwa toka Comoro na wako tayari kuwa na kliniki za ufuatiliaji kwenye visiwa hivyo.“Kwa idadi yao na inavyoongezeka,tunakusudia tuwe na wadi maalum ya wanaotoka Comoro katika siku za karibuni,” alisema Prof Janabi.

Kwa upande wake,Balozi Yakubu aliahidi kwenda kufanyia kazi na kuwa na uratibu mzuri wa wananchi wa Comoro kuja nchini kwa matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news