Mzabuni hatiani kwa hongo wilayani Bukoba

KAGERA-Mahakama ya Wilaya Bukoba mkoani Kagera imemtia hatiani mzabuni,Consolatha John Balole ambaye ni Meneja wa Kampuni ya ZainAbbas Enterprises.
Picha na LN.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, kwa kosa la hongo alilolitenda kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (b) PCCA.

Hukumu hiyo dhidi ya Consolatha John Balole katika shauri la rushwa Namba 13177/2024 imetolewa Mei 17,2024 na Mheshimiwa Hakimu Flora Kaijage wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba.

Ilidaiwa kwamba kati ya mwezi Machi na Septemba,2022 mshitakiwa alijipatia manufaa isivyo stahili hongo ya shilingi milioni 15. 54
katika manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, fedha ambayo amekwisharejesha katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera.

Hata hivyo, mshtakiwa amelipa faini na kuachiwa huru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news