Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi ampa kongole Rais Dkt.Samia

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Bw Ludovick Nduhiye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza na kukamilisha miradi katika sekta ya ujenzi.
Ametoa shukrani hizo leo Mei 28,2024 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma wakati akifunga maonesho ya siku mbili ya Wizara ya Ujenzi pamoja na taasisi na wakala zake, ambayo yalikuwa na lengo la kuonyesha kazi zilizofanywa na zinazoendelea kufanyika katika sekta ya Ujenzi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Nduhiye amesema kuwa, Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu tangu ameingia madarakani amefanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa na midogo huku miradi mingine ikiwa inaendelea kwa kasi kubwa.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba na majengo ya serikali, miundombinu ya Barabara, Madaraja, Viwanja vya ndege na vivuko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news