DAR-Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetangaza kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita na ualimu huku likitoa rai kwa kamati za mitihani kuhakiksha usalama wa vituo vya mitihani unaimarishwa na vituo vinatumika kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na baraza hilo nchini.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Said Mohamed ameyasema hayo leo Mei 5,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.
Mohamed amesema,mtihani huo unatarajiwa kuanza Mei 6 na kukamilika Mei 24,2024.
“Mitihani ya Kidato cha Sita (ACSEE) na Ualimu ngazi ya cheti na Stashahada itaanza rasmi Mei 6 kwa Tanzania Bara na Zanzibar ambapo wa kidato cha sita utakamilika Mei 24 wakati wa ualimu utakamilika Mei 20 mtihani wa kidato cha sita utafanyika katika shule za sekondari 931 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 258 na vituo vya ualimu 99;