DODOMA-Nelson Memorial Secondary School iliyopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imeendelea kuwa kinara katika nidhamu na matokeo wilayani humo.
Pia, shule hiyo imeendelea kuwa kivutio kwa wazazi na walezi wengi kutokana na namna ambavyo imekuwa ikitoa huduma bora kuanzia elimu, malezi na maadili.

Cheti hicho kilichotolewa Februari 16, 2024 kimesainiwa na Afisa Elimu Sekondari wilayani humo, Benadetha Thomas na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, Mwanahamisi H. Ally.
Shule hiyo ambayo ina usajili Na.S5879 ambayo ni ya bweni kwa wavulana na wasichana kipaumbele chao ni nidhamu na taaluma.