OUT yatoa huduma bora Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga

TANGA-Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania kinashiriki kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza tarehe 25/05/2024 jijini Tanga.
Karibuni sana kwenye Banda la Maonesho la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mjipatie huduma zifuatazo:

Mosi:Udahili na usajili wa masomo katika ngazi mbalimbali kuanzia Astashahada, Stashahada, Shahada, Umahiri na Uzamivu.

Pili:Bunifu mbalimbali ambazo zimefanywa na OUT kwa lengo la kutatua changamoto za jamii na kukuza ajira kwa jamii. Takribani Bunifu 10 zinaoneshwa kwenye maonesho haya hapa Tanga.

Tatu:Tafiti kutoka kwa watafiti wanataaluma wa OUT ambazo kwa hakika zinasaidia katika kuleta maendeleo nchini katika sekta za elimu, afya, lishe, ujasiariamali, mazingira, uchumi wa buluu, utalii na ukarimu, ustawi wa jamii na utawala.

Nne: Huduma za Teknolojia saidizi kwa watu wenye mahitaji maalumu. OUT inatoa mafunzo ya TEHAMA bure kwa watu wote wenye mahitaji maalumu ikiwemo wasioona na wasiosikia.

Makundi haya yanaweza kuwasiliana na kusoma taarifa na habari mbalimbali katika mitandao ya kijamii, vitabu na machapisho mbalimbali. Njooni kwenye Banda mjionee wenyewe huduma hii adhimu inayotolewa na OUT.

Tano:Mifumo mbalimbali ya ufundishaji na ujifunzaji inayotumiwa na OUT katika kutoa elimu kwa njia za Masafa, mtandao na Huria. Mifumo hiyo ni MOODLE yaani mfumo wa ujifunzaji Kielektroniki, mihadhara kwa njia ya ZOOM, VIMBWETTE vya ZOOM, Telegram, WhatsApp, mafunzo ya ana kwa ana, mafunzo kwa vitendo na ufanyaji wa mitihani kupitia mifumo ya kawaida pamoja na ODEX yaani kuomba mtihani wakati wowote mwanafunzi anapokuwa tayari. Njooni bandani tuwapatie huduma hizi na nyingine.

Sita:Njooni tuwaeleze kuhusu ulipaji wa ada kidogo kidogo kadri ya uwezo wa mwanafunzi, kusoma ukiwa popote na ukihama unaendelea kusoma ukiwa huko ulipohamia, kuhitimu masomo yako pale unapomaliza na kupata vyeti vyako bila kuchelewa.

Pia, tutakueleza kwamba ukitaka kupumzika unaruhusiwa na ukiwa tayari unarudi na kuendelea pale ulipokuwa umeishia. Njooni tuwaeleze kwamba OUT mambo ni mazuri sana unasoma bila vikwazo vyovyote.
Saba:Program ya Foundation kwa wahitimu wa kidato cha Sita na Diploma kwa lengo la kukamilisha vigezo vya kujiunga na shahada ya kwanza. Programu hii ipo hapa OUT kwa wote wenye sifa stahiki.

Haya na mengine mengi tumekuandalia kwenye Banda letu la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania hapa kwenye Maonesho jijini Tanga. Karibuni sana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news