Poland yaahidi ushirikiano Elimu Ujuzi nchini

DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo tarehe 17 Mei, 2024 amekutana na Balozi wa Poland nchini Tanzania, Mhe. Krzystof Buzalski ambapo wamezungumzia kuhusu kuendelea kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika Sekta ya Elimu.
Katibu Mkuu Nombo amemueleza Balozi huyo kuwa, Tanzania inafanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo kutilia mkazo elimu ya amali inayolenga kujenga ujuzi kwa vijana ili washiriki kikamilifu katika maendeleo kupitia nyanja mbalimbali za uzalishaji.
Prof. Nombo ameiomba Poland kushiriki kwa namna mbalimbali katika kutekeleza mageuzi hayo, kwani yanahitaji rasilimali za kutosha ikiwemo fedha na wataalam katika eneo la kiufundi ili kufikia malengo yanayotarajiwa.
Mhe. Buzalski ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ya elimu na kuanza utekelezaji wa Sera na Mitaala mipya ya Elimu na kuahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news