KAGERA-Polisi wilayani Missenyi wametakiwa kuwa mabalozi kwa wananchi wanaowazunguka ili kuwafikishia elimu ya masuala ya fedha waliyoipata kutoka kwa Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha iliyoko katika kampeni ya kutoa elimu ya fedha kwa umma katika mikoa mbalimbali nchini.

“Tunaahidi kuwaelimisha Polisi wengine ambao hawajapata elimu hii, lakini pia tutawajengea uwezo Polisi Jamii ili wawaelimisha wananchi ambao wapo karibu nao ili waepukanane na mikopo umiza,” alisema SP Soa.
Alisema kuwa elimu ikiwafikia wananchi wote nchini itaisaidia Serikali kupondokana na kupunguza migogoro ya kesi mbalimbali zinazoendelea kwenye Vituo vya Polisi kuhusu mikopo inayowakumba wananchi mbalimbali.
Naye Mkaguzi wa Polisi Baraka Mafwimbo, aliiomba Serikali kuongeza nguvu ya kudhibiti na kuimarisha mifumo ya Taasisi zinazohusika na utunzaji wa taarifa binafsi za wananchi kuhakikisha zinalinda taarifa hizo ili kuepusha taarifa hizo kufikiwa na watoa huduma ya mikopo na kuweza kuwashawishi kukopa fedha.
“Binafsi nimewahi kupigiwa simu na kushawishiwa kuchukua mkopo na watoa huduma ambao sikujua taarifa zangu wamezitoa wapi, lakini walikuwa wananielezea kama wananifahamu lakini hawakuweza kufanikiwa kwa kuwa nimewahi kupata elimu ya masuala ya fedha zamani,"alisema Mafwimbo.

