Prof.Nombo aridhishwa na ujenzi wa VETA wilayani Muheza

TANGA-Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo ameridhishwa na kazi inayoendelea ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA cha Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Prof. Nombo akikagua ujenzi wa chuo hicho Mei 15, 2024 amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na kushirikiana kikamilifu na msimamizi wa mradi huo ili kukamilisha kwa wakati.

Chuo hicho ni moja kati ya vyuo 64 vya VETA wilaya vinavyoendelea kujengwa nchini ambapo katika Chuo cha Muheza ujenzi unahusisha majengo tisa ikiwemo jengo la utawala, madarasa na karakana nne za ufundi seremala, uashi, umeme na ufundi bomba.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Dr. Jumaa Mhina ameipongeza Serikali na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kujenga Chuo hicho ambacho kitaleta chachu ya maendeleo katika Wilaya kwa kuwajengea Vijana ujuzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kiwanda FDC,Bw. Jofrey Mwiga amesema ujenzi umefikia asilimia 38.1 ambapo Chuo hicho kitakapo kamilika kitachukua wanafunzi zaidi ya eflu 2

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news