Rais Dkt.Mwinyi akaribisha wawekezaji kutoka Ufaransa

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito na kuwakaribisha wafanyabiashara kutoka Ufaransa kuangalia fursa kuwekeza Zanzibar katika maeneo mbalimbali. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Mei 29,2024 alipofungua mkutano wa majadiliano ya fursa za uwekezaji kati ya Ufaransa na Zanzibar kutoka kwa ujumbe wa wafanyabiashara wa makampuni 20 ya Ufaransa katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatty Zanzibar.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema, sera kuu ya uchumi wa Zanzibar ni uchumi wa buluu hivyo amewakaribisha kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya utalii wa fukwe, 

Pia, urithi, michezo na mikutano, sekta ya bandari, mafuta na gesi, sekta ya bandari ikiwemo ya makontena , uvuvi pamoja na meli za usafirishaji wa mizigo na abiria.

Amebainisha fursa za miradi ya miundombinu ikiwemo barabara, viwanja vya ndege , sekta ya nishati na maji, pamoja na kilimo cha viungo.

Rais Dkt.Mwinyi amewahikikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira mazuri kikamilifu ya kufanya biashara na uwekezaji.
Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.Nabil Hajlaoui , Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe.Ali Mwadini na Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la MEDEF kutoka Ufaransa, Gerald Wolf.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri na sekta binafsi wameshiriki mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news