Rais Dkt.Mwinyi akutana na Askofu Mkuu wa Aglikana Duniani,Justin Welby

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Kianglikana na Taasisi nyingine za dini kwa kudumisha amani na utulivu.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana Duniani , Askofu Mkuu Justin Welby na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar leo Mei 11,2024.

Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Askofu Justin Welby kwa ujio wake Zanzibar.
Naye Askofu Justin Welby amempa pole Rais Dkt.Mwinyi kutokana na kifo cha Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi

Vile vile ujumbe huo umempongeza kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Rais Dkt.Mwinyi atashiriki kesho Ibada ya Maridhiano kutokana na madhila waliyofanyiwa Waafrika wakati wa Biashara ya utumwa katika Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini itakayoongozwa na Askofu Mkuu, Mhashamu Justin Welby.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news