ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Mhe.Sharrif Ali Sharrif kuwa mjumbe wa Tume ya Mipango ya Zanzibar.
Uapisho huo umefanyika Mei 26,2024 katika Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. Mhe.Sharrif Ali Sharrif ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji wa SMZ.