Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali na Mashirika ya Umma yaliyo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Katika taarifa iliyotolewa Mei 9,2024 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said imebainisha kuwa, Arafat Ally Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Kabla ya uteuzi huo Arafat alikuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) pia ni Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Pia, amemteua, Balozi Omar Yussuf Mzee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Balozi Omar ni Mstaafu katika Utumishi wa Umma.

Dkt.Huda Ahmed Yussuf ameteuliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Naye, Saleh Saad Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), kabla ya uteuzi huo, Saleh alikuwa Msaidizi Mkurugenzi Huduma za Uwekezaji ZIPA.

Dkt.Haji Gora Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kitaifa na Uratibu wa Diaspora katika Ofisi ya Rais Ikulu.

Kabla ya uteuzi Dkt. Haji alikuwa Mkuu wa Divisheni ya Mipango, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Taarifa hiyo ya Katibu Kiongozi imefafanua kuwa, uteuzi huo unaanza Mei 9, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news