Rais Dkt.Mwinyi atoa maagizo Ripoti ya CAG

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itafanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika ripoti ya CAG na kuunda kamati maalum itakayoshughulikia kasoro za kiutendaji zinazotokana na hoja za CAG kila mwaka.Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi, Zena Ahmed Said kuunda kamati hiyo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Mei 13,2024 baada Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Dk.Othman Abbas Ali kuwasilisha ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2022/23 iliyofanyika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ameendelea kusisitiza kuheshimiwa Ofisi ya CAG na kutoingilia kwa mujibu wa katiba katika kutimiza majukumu yake kwa uhuru.
Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ameridhika kwa hatua za mafanikio ya zaidi ya asilimia 90 ya hati za ukaguzi zinazoridhisha katika ripoti ya mwaka 2022/23.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Serikali ikijikita kujiendesha kwa njia ya mifumo ya kidijitali katika kila nyanja itasaidia kupiga hatua za maendeleo kwa haraka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news