Rais Dkt.Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka Korea

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka Korea kuja kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi wa buluu, ujenzi wa kumbi za mikutano ya kimataifa.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Kudumu ya Bunge la Korea,Mhe.Sul Hon na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar leo Mei 11,2024.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Korea kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya sekta ya elimu, afya, uvuvi na mengineyo.
Kwa upande mwingine,Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru ujumbe huo kwa kuitembelea Zanzibar. Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe.Kim Sun Pyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news