ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Mhe.Gustavo Martins Nogueira na ujumbe wake Ikulu jijini Zanzibar kwa kujitambulisha leo Mei 13, 2024.
Katika mazungumzo yao wamegusia kuendeleza uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Brazil katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, barabara, uwanja wa ndege wa Pemba, utalii, fursa za uwekezaji wa mafuta na gesi Zanzibar, na biashara hasa ya sukari.