Rais Dkt.Samia aahidi mema zaidi kwa wasanii nchini

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameahidi mema zaidi kwa wasanii na wanamichezo nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya, Rajab Abdul (Harmonize) katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa ahadi hiyo usiku wa Mei 25,2024 wakati akishiriki uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya, Rajab Abdul maarufu kama Harmonize ndani ya ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Vijana wa sanaa zote na michezo mpo katika moyo wangu na jukumu langu ni kuijenga kesho yenu bora.
Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul (Harmonize) akitumbuiza katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Albamu yake ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye ukumbi wa Mlimani City kushuhudia uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama ya Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul (Harmonize) tarehe 25 Mei, 2024.

"Niwasihi endeleeni kushirikiana na Serikali na kufanya kazi zenu kwa bidii na maarifa zaidi, kubwa zaidi acheni maugomvi.

"Acheni kuzodoana, saidianeni, vutaneni mkue kwa pamoja, mkikua wengi zaidi Tanzania imekua zaidi,"amesisitiza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul (Harmonize) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul (Harmonize) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Flavour Rajab Abdul (Harmonize) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amesema, “Tunapofungua nchi wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua wasanii.

“Nataka nifuatane na wasanii inategemea ratiba yangu kule ninakokwenda,lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba wasanii.

"Lakini zaidi nitakuwa na safari keshokutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa wasanii wetu hasa waigizaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Flavour Rajab Abdul (Harmonize) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Mzazi wa Msanii wa Bongo Flavour, Harmonize, Habiba Baisa Chivalavala wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Mzazi wa Msanii wa Bongo Flavour Harmonize, Habiba Baisa Chivalavala wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

“Tunakwenda Korea na mnawajua ni wazuri sana kwa kuigiza, michezo yao naona inatambatamba kwenye TV zetu.

"Kwa hiyo tunaenda kutafuta nafasi za mafunzo na nadhani tutafanikiwa,"ameongeza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news