DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua, Dkt. Elirehema Joshua Doriye kuwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 6,2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Vile, Rais Dkt.Samia amemteua Christopher Derek Kadio kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Kadio anachukua nafasi ya Esther Hellen Lugwisha ambaye amemaliza muda wake kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Tags
Breaking News
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro
Habari
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali