Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA),Mhe. Dkt. Fatih Birol pamoja na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa akiwa Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afrika. Rais Samia anashiriki Mkutano huo wa Kimataifa tarehe 14 Mei, 2024.Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.