Rais Dkt.Samia ateua sita

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali Mei 29,2024.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus imefafanua, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Dkt. Mursali Ally Milanzi kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Mipango ya Kitaifa.

Kabla ya uteuzi huu Dkt.Milanzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Kitaifa katika Tume ya Mipango.

Vile vile Rais Dkt.Samia amemteua Dkt.Lorah Basolile Madete kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Ubunifu wa Biashara ambapo kabla ya uteuzi huu alikuwa Meneja wa Idara ya Uchumi Benki Kuu ya Tanzania, Tawi la Mwanza.

Rais Dkt.Samia pia amemteua Dkt.Linda Ezekiel kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango anayeshughulikia masuala ya Menejimenti ya Utendaji na Tathmini ambapo kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, President’s Delivery Bureau (PDB).

Wakati huo huo,Rais Dkt.Samia amemteua Alban Mark Kihulla kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), kabla ya uteuzi huu Bw. Kihulla alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Pia, amemteua Prof. Najat Kassim Mohamed kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), kabla ya uteuzi huu Prof. Najat alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo (Mipango, Utawala na Fedha), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Rais Dkt.Samia amemteua Bernadetta Nagonyani Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Bernadetta ni Mkurugenzi wa Mafunzo mstaafu, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news